ASSEMBLY OF BELIEVERS CHURCH



ABC GLOBAL CHURCH

ONE DAY SPECIAL RETREAT
APOSTLE ALLEN KIPANGULA
SESSION THREE
SOMO : NAFASI YA KUISHI MAISHA MATAKATIFU KWENYE KULETA NYAKATI ZA KUBURUDISHWA.
31.12.2025

Matendo ya Mitume 3:19
[19]Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;

-Ni mapenzi ya Mungu tushinde dhambi na kuishi mbali na hofu ya dhambi.

MALENGO YA SOMO

1. Kupokea imani ya kuwa inawezekana kuishi maisha matakatifu duniani

2. Kupokea uwezesho wa kuishi maisha matakatifu

3. Kupokea neema itakayokujenga kwenye kuishi maisha matakatifu
Matendo 30:32

4. Kupata faida za kuishi maisha matakatifu

UTAKATIFU NI NINI!?
Ni hali ya kutengwa kwaajili ya matumizi maalumu ya Mungu

Kutoka 30:30
Nawe utawatia mafuta Haruni na wanawe, na kuwatakasa, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.
-Mungu ni mtakatifu, hivyo watumishi wake wanapaswa kuwa watakatifu.

Utakatifu sio dhambi tu, ni zaidi ya dhambi na nikujua kuwa wewe umetengwa kwaajili ya Mungu na kwa niaba ya Mungu

KUISHI MAISHA MATAKATIFU NI NINI
Ni kuishi, kuwaza,kunena na kutenda kwaajili ya Mungu
Waefeso 2:10
[10]Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.

Kuishi maisha matakatifu ni kukubali kuwa chini ya Neno, na kuendeshwa na Roho Mtakatifu
Ezekieli 36:27

Kuishi maisha matakatifu ni kumruhusu Mungu mtakatifu adhihirike kupitia maisha yako
Wagalatia 2:20
Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.

NINI AMBACHO KINAZUIA WATU WASIISHI MAISHA MATAKATIFU
Udanganyifu wa dhambi
Waebrania 3:13
[13]Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
-udanganyifu kwamba wote wanatenda dhambi!
Ayubu 1:1
[1]Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.
-Inawezekana hata wengine wakawa wachafu,lakini kila mtu atasimama peke yake!

Udanganyifu mwingine ni kuwa hakuna mtakatifu duniani
Waefeso 1:1
[1]Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu; kwa watakatifu walioko [Efeso] wanaomwamini Kristo Yesu.

Zaburi 16:3
Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora,
Hao ndio niliopendezwa nao.

Udanganyifu wa tatu ni dhambi inapofusha watu wasione madhara kwa wakati huo
Mithali 14:12
Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu,
Lakini mwisho wake ni njia za mauti.

Udanganyifu wa nne dhambi itakufanya uone ni kama jambo la kawaida.

Waefeso 4:18-19
[18]ambao; akili zao zimetiwa giza, nao wamefarikishwa na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao.
[19]ambao wakiisha kufa ganzi wanajitia katika mambo ya ufisadi wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani.

Dhambi itakufanya uchukie watu wanaohubiri maisha matakatifu,na wanaoishi.
Mwanzo 4:7
[7]Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.

NAFASI YA MUNGU NA NAFASI YAKO KATIKA KUISHI MAISHA MATAKATIFU
-Ni lazima umruhusu Mungu akutakase, kisha ujitakase.

KUTAKASWA NA MUNGU
1 Petro 1:2
[2]kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.

KUJITAKASA
2 Timotheo 2:20-21
[20]Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina.
[21]Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema.

-Mungu akikutenga kama wewe hautojitenga, haitakusaidia kitu.

2 Wakorintho 6:17
[17]Kwa hiyo,
Tokeni kati yao,
Mkatengwe nao, asema Bwana,
Msiguse kitu kilicho kichafu,
Nami nitawakaribisha.

-Kujitenga ndio humpa mtu upako wa ndani.

NGUVU YA KUTAKASWA NA MUNGU
1 Petro 2:24
[24]Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.

Warumi 8:3-4
[3]Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili
[4]ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.

• Yesu yupo tayari kutupa neema kila anayehitaji kushinda dhambi
Tito 2:11-12
[11]Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
[12]nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa.

• Yesu yupo tayari kumpa mtu Roho wake mtakatifu
• warumi 1:1-4

KUJITAKASA
• Kama kuna dhambi ambayo inakutesa amua kujiweka wazi kwa Mungu na kwa mtu wa Mungu.
• Yakobo 5:16
[16]Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
• Amua kujaza neno la Mungu ndani yako
Zaburi 119:11
[11]Moyoni mwangu nimeliweka neno lako,
Nisije nikakutenda dhambi.

• Linda milango ya moyo wako( macho yako)
• linda masikio yako
1corintho 15:33
• Jikite kwenye vitu vinavyolisha maono yako,kusudi lako.
Mithali 29:18
[18]Pasipo maono, watu huacha kujizuia;
Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.

FAIDA ZA KUISHI MAISHA MATAKATIFU
1. Unalindwa dhidi ya nguvu za giza na utendaji wake.
Yohana 5:14, Ayubu 1:10

2. Maisha matakatifu yatakupa mamlaka ya kiungu
Ufunuo wa Yohana 22:14
[14]Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.

Danieli 4:17
[17]Hukumu hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge.

1 month ago | [YT] | 27

ABC GLOBAL CHURCH

UNGANA NA SISI KUMSHEREKEA PASTOR WETU WA Abc Global Church HQ PASTOR Joseph Makindi

TUANDIKIE KWENYE COMMENT AMEFANYIKA BARAKA KWAKO KWA NAMNA GANI.!?

ZAWADI AU SADAKA YAKO UNAWEZA KUIWASILISHA KWA NAMBA 0759625673

SISI TUU ISHARA NA AJABU

1 month ago | [YT] | 34

ABC GLOBAL CHURCH

Merry Christmas

1 month ago | [YT] | 14

ABC GLOBAL CHURCH

MAONO KAMA MTAJI WA MAISHA

MAONO
1. Ni picha ya mambo yaliyopo kwenye moyo wa Mungu anayotaka yawe halisi duniani (Mapenzi yake yaliyo mbinguni, anayotaka yafanyike halisi duniani)
Mathayo 6:9-10
2. Maono ni kazi kamilifu mbinguni inayoletwa kwenye moyo wa mtu ili izaliwe kwenye uhalisi hapa duniani
Wafilipi 1:6
●Mungu ni mfanyakazi, anafanya vitu kwanza rohoni, kisha anamtafuta mtu mwaminifu wa kuviweka moyoni mwake ili avizae kwenye uhalisi
●Kazi alizofanya Mungu tayari mbinguni ndio huja duniani kwa mfumo wa picha za moyoni, na hizo picha ndizo huitwa mawazo
●Kila ukipata wazo chanya, la maendeleo, umekamata sauti ya Mungu kwa mfumo wa picha (Yeremia 1:11-12)
●Kila ukipata wazo, tayari umepata kazi iliyokamilika rohoni na wewe ni tumbo tu la kuizaa kwenye uhalisia
Isaya 26:18

3. Maono ni upeo wa kuona wa mtu kutoka katika picha kubwa ya Mungu
Mwanzo 13:14-15
●Ibrahim aliona ulimwengu akapewa kuwa mrithi wa ulimwengu (Warumi 4:13)
● Ukubwa wa maisha ya mtu huwa sawa na upeo wake wa kuona
"Kwa kadri macho yako yatakavyoona, nitakupa" (As far as your eyes can see)
-Kuona ndio mtaji mkubwa kuliko yote kuelekea ukuu
-Hakuna atakayekwenda umbali ambao macho yake hayajawahi kwenda
-Taa ya mwili ni macho, kule ambako macho ya moyo wako hayajafika, maisha yako hayatafika

4. Maono ni picha ya anavyojiona mtu nafsini mwake
Mithali 23:7
●Vile unavyotakiwa kuwa tayari Mungu ameshaiweka moyoni mwako kama picha fulani
●Ni waliofanikiwa kuchungulia ndani yao na kujiona wao halisi, ndio huwa watu wa maana kwenye maisha haya
●Muujiza mkubwa anaoweza Mungu kumpa mtu ili abadilike kimaisha ni kumsaidia kuona uwezo aliobeba ndani yake
Waamuzi 6:11-16
●Hakuna mtu asiye na talanta ndani yake, changamoto yetu kubwa ni kutoziona, kuzitambua na kuziishi kwa kiwango cha juu

SIFA ZA MAONO
1. Chanzo chake ni Mungu mwenyewe
2. Ni kazi iliyokamilika mbinguni
3. Huwekwa moyoni mwa mtu kama picha au wazo
4. Hupewa mtu mmoja, lakini yanaweza kugusa na kuathiri dunia nzima
5. Yanahitaji imani ili yatimie (Kwa Mungu, kwa maono yenyewe na kwa mhusika/ kujiamini)
6. Yanahitaji watu sahihi walioumbwa kuyabeba na wewe
7. Rasilimali huja njiani kadri mtu anavyoanza anapoweza kuelekea anapotakiwa (chukua hatua)
8. Maono hupanuka kadri mtu anavyochukua hatua na kufanya

2 months ago | [YT] | 18

ABC GLOBAL CHURCH

KWELI TANO KUHUSU UTAJIRI NA UMASIKINI

1. HAKUNA ANAYEZALIWA TAJIRI AU MASIKINI, WOTE TUNAZALIWA TUKIWA NA NAFASI SAWA

i) Wote tunazaliwa uchi lakini hatuzaliwi watupu, tunazaliwa na vitu ndani yetu vinavyotosha kugeuza maisha yetu tukivitumia

ii) Uamuzi wa kubaki uchi unabaki mikononi mwa mhusika akishajitambua

2. UMASIKINI AU UTAJIRI SI MUUJIZA BALI NI MATOKEO YA MAAMUZI SAHIHI AU MABOVU MENGI ANAYOFANYA MTU

Maisha ni mchezo wa maamuzi ambao mtu anaucheza kwa masaa 24 (siku moja moja) ya maisha yake kila siku!
Maamuzi kuhusu FURSA, MUDA, RASILIMALI, FEDHA INAYOPITA MIKONONI MWA MTU NA MAHUSIANO NA WATU, hivi ndivyo huamua mtu awe masikini au tajiri baada ya kipindi fulani cha muda!

3. UMASIKINI AU UTAJIRI SI BAHATI NZURI AU MBAYA, MTU ANAKUWA TAJIRI AU MASIKINI KWA MAAMUZI YAKE YA DHATI YANAYOJIRUDIA!

Hakuna masikini aliyekuwa MASIKINI bahati mbaya, kila masikini anavunja KANUNI ZINAZOTAWALA MAISHA kwa mwendelezo na mfululizo!
Na kila TAJIRI anatajirika kwa kuzizingatia na kuziheshimu KANUNI ZINAZOTAWALA MAISHA ambazo masikini anazivunja!

4. MTU YEYOTE ANAWEZA KUANZIA ALIPO NA KUWA TAJIRI AU MASIKINI

TAJIRI anaweza kuamua kuishi kiholela nje ya KANUNI na baada ya muda mchache akawa masikini kabisa, kadhalika MASIKINI anaweza kugeuka na kuanza kuziheshimu KANUNI ZINAZOTAWALA MAISHA na baada ya MUDA atakuwa tajiri!
UMASIKINI na UTAJIRI ni kama vazi ambalo mtu yeyote anaweza kulivaa au kulivua apendavyo mwenyewe!

5. UMASIKINI AU UTAJIRI HAUTEGEMEI SANA MAHUSIANO BINAFSI NA MUNGU BALI UWEZO WA MTU KUZIISHI KANUNI ZA MUNGU ZINAZOTAWALA MAISHA

Mfano Bakhresa au Mo Dewji hawajajaa maandiko, kunena kwa lugha, wala karama za Roho Mtakatifu, lakini NI MATAJIRI NA KUNA UWEZEKANO HADI YESU ANARUDI WATAKUWA WANAZIDI KUTAJIRIKA!

Lakini watu hawa WANAISHI KANUNI zinazotawala maisha kama vile UTENDEAJI KAZI MAWAZO (Believing and working on every positive and constructive idea), BIDII YA KAZI (Hardwork), MATUMIZI SAHIHI YA FURSA (The best use of opportunities), MAHUSIANO SAHIHI NA WATU (They know how to relate with people based on their levels importance, status and positions), MATUMIZI SAHIHI NA BORA YA MUDA (Rightly investing, utilizing and redeeming time), na NYINGINE NYINGI....

NIMESHAKUPA PA KUANZIA,

JIFUNZE NA UAMKE,

CHAGUA UPANDE WAKO KATI YA UMASIKINI AU UTAJIRI,

HALAFU TUONANE MIAKA MITATU, MITANO AU KUMI IJAYO KAMA BWANA YESU HATAKUWA AMERUDI KULICHUKUA KANISA LAKE!

RUKSA KUSHARE HII POST HASA NA WATU WALIOOKOKA WENGI UNAOWAFAHAMU ILI TULIAMSHE KANISA...

YOUTUBE: Pastor Dickson Kabigumila
(Video zaidi ya 600)

9 months ago | [YT] | 14

ABC GLOBAL CHURCH

RETREAT CAMP AT ABC GLOBAL HQ - KINZUDI, DECEMBER 2024
UJUMBE: KUINUKA KWA WAOKOZI- OBADIA 1:21

NUKUU ZA UFUNGUZI WA KAMBI

MHUDUMU: MWALIMU Francis Langula
DAY O1: 26.12.2024

1 year ago | [YT] | 4

ABC GLOBAL CHURCH

RETREAT CAMP FUNGA MWAKA 2024 NA KUFUNGUA MWAKA 2025

MASHUJAA WANAINGIA KAMBINI TAYARI

UNASUBIRIWA WEWE TU

KESHO SAA 1:00 ASUBUHI TUNAANZA RASMI KAMBI HII YA KUMUINULIA MUNGU WAOKOZI SAWA NA OBADIA 1:21

1 year ago | [YT] | 3

ABC GLOBAL CHURCH

RETREAT CAMP FUNGA MWAKA 2024 NA KUFUNGUA MWAKA 2025

MASHUJAA WANAINGIA KAMBINI TAYARI

UNASUBIRIWA WEWE TU

KESHO SAA 1:00 ASUBUHI TUNAANZA RASMI KAMBI HII YA KUMUINULIA MUNGU WAOKOZI SAWA NA OBADIA 1:21

1 year ago | [YT] | 7

ABC GLOBAL CHURCH

SADAKA ZA OVYO MAGROUP YA WHATSAPP ZA WATUMISHI WA MUNGU

1. Sadaka za kuingia na kubaki kwenye group la mtumishi za lazima,
Mfano, kila anayeingia kwenye group alipie 5000, na kila mwezi atoe sadaka ya kuendelea kubaki kwenye group 2000

Ebu acheni hii michezo mara moja,
Biblia imetupa kanuni za utoaji,
A. Iwe kwa moyo wa kupenda
B. Iwe kwa moyo wa kuchangamka
C. Iwe kwa hiari na si kulazimisha
D. Kila kitu kifanywe bila manung'uniko wala lawama

Watu wanalalamikia mno kile kinachoendelea kwenye magroup ya Whatsapp ya watumishi wengi wa kweli wa Mungu, ambao nao WANAINGIA TARATIBU KWENYE MTEGO WA KUPENDA FEDHA NA KUBUNI MBINU ZA KUIKUSANYA ISIVYO HAKI!

2. Wana group wa Whatsapp kukununulia nguo zako (suti, viatu, na vya kuvaa kanisani kwako ibadani),
Tamaa ya kutaka kuvaa nguo mpya kila ibada itawaharibu wahudumu wengi wa Injili,
Kwanini msitosheke na nguo mlizonazo na kuzirudia hata kama ni kila Jumapili?
Kwanini msimwamini Mungu avikaye maua ya kondeni kuwavika enyi wa imani haba? Mnahubiri Mungu anaweza kuvika maua lakini hamuamini anaweza kuvika wavunaji wa roho za watu kwenye Ufalme?
Unashusha heshima, utu na jina ulilopata kwa taabu kwa shilingi 2000, 5000 au 10,000 inayotolewa kwa lawama? AU WENZETU NINYI HAMJALI TENA WATU, ONLY GOD CAN JUDGE YOU? MKIENDELEA NA MSIGEUKE, MTASHANGAA WATU WATAKAVYOJIONDOA KUWAPA HATA 100 TU KUANZIA LEO!
Acha Mungu aguse watu wakupe mahitaji kwa hiari, NA WEWE ISHI KWA IMANI KAMA UNAVYOFUNDISHA IMANI!

3. Semina za kulipia 5000, 10,000, 20,000 hadi 50,000 kwa wiki au mwezi,
Mnenaji anadai ametumia muda kukusanya nondo atakazotema mle ndani!
Anadai anatumia muda wake wa muhimu kuwafundisha, hivyo waulipie!
Wewe huna ubongo wako ni wa Mungu, huna muda wako umepewa bure uutumie kutumikia watu wa Mungu! ACHENI UTOZAJI WA PESA KWENYE HUDUMA ZA KIROHO, MKIENDELEA MTAJIONEA WATU WATAKAVYOJITOA HUKO KAMA WANAKIMBIZWA, NA TAA ZENU ZITAFIFIA NA MAJINA YATAPOTEZA MVUTO!

Askofu Dickson Kabigumila
ABC GLOBAL DUNIANI
08.08.2024

1 year ago | [YT] | 17

ABC GLOBAL CHURCH

A man who says sorry when he is wrong is HONEST

A man who says sorry when he is not sure if he is wrong is WISE

A man who says sorry even when he knows is right is A HUSBAND

To ladies and women out there...

1 year ago | [YT] | 26