Video za habari na matukio duniani kutoka BBCSwahili.com


BBC News Swahili

Mataifa haya yanagombea kuwa wa kwanza kufika mwezini

19 hours ago | [YT] | 0

BBC News Swahili

Kardinali wa pili Tanzania Polycarp Pengo, 82, alipadrishwa mwaka 1971. Kufahamu zaidi tembelea www.bbc.com/swahili/live/cm2x39kp5j1t

19 hours ago (edited) | [YT] | 44

BBC News Swahili

Mdogo wake na Mfalme Charles wa Uingereza Andrew Mountbatten amekamatwa kwa tuhuma za utovu wa nidhamu katika ofisi ya umma huku polisi wakichunguza madai kwamba alishiriki habari za siri na Jeffrey Epstein aliyepatikana na hatia uhalifu wa kingono.
Pangusa kushoto kwa taarifa zaidi:
www.bbc.com/swahili/live/c9wn8vx8lndt
#bbcswahili #mfalme #mwanafalme #epstainfiles

1 day ago | [YT] | 22

BBC News Swahili

Mashahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa chama cha upinzani nchini Tanzania wanaendelea kutoa ushahidi katika kesi hiyo. kusoma zaidi bofya www.bbc.com/swahili/live/c9wn8vx8lndt

1 day ago | [YT] | 84

BBC News Swahili

Watu wasiopaswa kufunga Ramadhan

1 day ago | [YT] | 0

BBC News Swahili

Kenya imekuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki kupokea Lenacapavir, dawa ya muda mrefu ya kinga dhidi ya VVU (PrEP) inayolinda watu wasiokuwa na VVU dhidi ya maambukizi.

2 days ago | [YT] | 56

BBC News Swahili

Kiongozi na mwasisi wa haki za kiraia Mchungaji Jesse Jackson amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84.

3 days ago | [YT] | 88

BBC News Swahili

Kesi ya kiongozi wa chama cha CHADEMA nchini Tanzania Tundu Lissu imeendelea ambapo Wakili upande wa serikali amesema wameleta mashahidi watatu ili kuendelea na usikilizwaji wa kesi. Kufahamu kwa kina kila kinachoendelea bofya www.bbc.com/swahili/live/cyv9em2r6njt

3 days ago | [YT] | 65

BBC News Swahili

Ukraine imeanzisha mpango unaowaruhusu wanajeshi kugandisha mbegu zao za kiume, huku nchi hiyo ikikabiliwa na tatizo la idadi ndogo ya watu kutokana na uvamizi wa Urusi.

Chini ya mpango huo, wanajeshi wa Ukraine wanaweza kuhifadhi mbegu za kiume bila malipo, na kuwapa wenzi wao chaguo la kupata watoto katika siku zijazo ikiwa wanajeshi watafariki dunia au wakiwa na msongo wa mawazo ama pengine wanapopata jeraha la muda mrefu lenye kuathiri uzazi wao.

Pangusa kushoto kwa taarifa zaidi:

www.bbc.com/swahili/live/cyv9em2r6njt
#bbcswahili #ukraineπŸ‡ΊπŸ‡¦ #russia #urusi #VIF #familia

3 days ago | [YT] | 26

BBC News Swahili

Kahawa inayozalishwa nchini Tanzania imeibuka kinara katika maonesho ya 22 ya African Fine Coffees Association (AFCA) 2026, kwa kushika nafasi ya kwanza barani Afrika na nafasi ya nne duniani kwa uzalishaji wa kahawa bora yenye ubora wa juu na iliyothibitishwa kuzingatia viwango vya uendelevu wa mazingira.

Maendeleo hayo yalitangazwa katika Ukumbi wa AICC jijini Addis Ababa, nchini Ethiopia, ambapo AFCA 2026 ilifanyika kuanzia Februari 4 hadi 6, 2026.
-
-
#bbcswahili #kahawa #coffee #ethiopia
www.instagram.com/p/DU2WHfzjotr/?img_index=1

3 days ago | [YT] | 110