⭐ OTV MEDIA – Official Channel"
OTV MEDIA ni channel ya burudani, comedy, interviews, muziki, lifestyle pamoja na kutatua changamoto za wananchi.
Tunatoa maudhui halisi, ya kuvutia na yenye kugusa jamii.
Karibu kwenye familia ya OTV MEDIA – Tumekufikia!
Subscribe ili uendelee kupata vipindi vipya kila siku.
📞 Wasiliana nasi:
📌 otvtanzania231@gmail.com
🎯 Lengo la OTV MEDIA:
Kuwa jukwaa la kusaidia vijana, wasanii chipukizi, wakina mama, na watu wanaopitia changamoto za kijamii kwa kuwapa nafasi ya kusikika, kuelimika na kuburudika.
OTV MEDIA
Rais Samia ametamatisha hotuba yake ya Bunge la 12 na kusema kuwa Bunge litavunjwa Agosti 3 2025
Bunge lilifunguliwa rasmi Novemba 1, 2020, likifunguliwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, hayati John Pombe Magufuli. Kuvunjwa kwa bunge hili kunafungua njia rasmi ya kuanza kwa mchakato wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
7 months ago | [YT] | 0
View 0 replies
OTV MEDIA
https://youtu.be/jnrgmg4vHCw
10 months ago | [YT] | 0
View 0 replies
OTV MEDIA
Halmashauri ya Jiji la Dodoma imejipanga kutoa huduma kwa wananchi wote kwakuzingatia mgawanyo wa Jimbo la Dodoma Mjini wenye mapendekezo ya kuligawa jimbo hilo kuwa Jimbo la Mtumba lenye kata 20 na Jimbo la Dodoma Mjini lenye kata 21.Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Dkt.Frederick Sagamiko, mara baada ya majadiliano na Madiwani kuhusu taarifa iliyowasilishwa na Afisa Uchaguzi wa Halmashauri yaJiji la Dodoma, Albert Kasoga kuhusu mapendekezoya mgawanyo wa Jimbo la Dodoma Mjini,wakati wamkutano maalumu wa Baraza la Madiwani uliofanyika Machi 12,2025."Mgawanyo huu kwa sasa unalenga mgawanyo wajimbo kuwa na Majimbo mawili, bado tutaendelea kuwa na halmashauri moja kwa maana ya utoaji huduma kwa ngazi ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma.Jiji litaendelea kuwajibika katika utoaji wa huduma katika majimbo yote mawili". amesema Dkt. Sagamiko Akizungumzia mgawanyo wa Jimbo la Dodoma Mjini,amesisitiza kuwa utazingatia zaidi kata na sio tarafa.
#OTVMedia #TUMEKUFIKIA #bosskitana
11 months ago | [YT] | 1
View 0 replies
OTV MEDIA
Tarehe 13.03.2025 muda wa saa 12:30 asubuhi huko katika maeneo ya mtaa wa njiro ndogo kata ya sokoni one katika halmashauri ya jiji la Arusha watu wawili wasiofahamika majina wanaume wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 28 walifariki dunia baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao na watu wasiofahamika.Watu hao walishambuliwa mara baada ya kuiba pikipiki iliyokuwa imeegeshwa Jirani na kituo cha mafuta cha simba oil kilichopo eneo la njiro ndogo ambapo pia walichoma pikipiki yenye nambaya usajili Mc 438 ESG aina ya Sinoray iliyokuwa inatumiwa na watu hao.Jeshi la Polisi Mkoani hapa linaendelea kufanya uchunguzi watukio hili ili kuibaini chanzo cha tukio na hatua zitachukuliwa kwawale watakaobainika kuhusika na tukio hili.Miili ya marehemu imehifadhiwa katika kituo cha Afya Murieti kwa ajili ya utambuzi nauchunguzi wa daktari.Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawaonya watu wanaoendelea kujichukulia sheria mkononi kuwa waache mara moja na badalayake watoe taarifa za uhalifu na wahalifu ili hatua sstahiki ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria.
11 months ago | [YT] | 0
View 0 replies
OTV MEDIA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Machi 11,2025 amekutana na Bi Martha ambaye siku za hivi karibuni amesikika kupitia mitandao ya kijamii kuwa anaidai Hospitali ya Rufaa ya Amana zaidi ya shilingi milioni 3 kutokana na kufanya kazi ya kushona nguo za chumba cha upasuaji na kusambaza pazia, kazi ambayo ilifanyika 2017 na 2021.
RC Chalamila amepata wasaa wa kufanya mahojiano na Bi Martha mbele ya waandishi wa habari na watumishi wa Hospitali ya Amana juu ya mchakato mzima wa madai hayo na kumtaka Bi Martha kuleta nyaraka zitakazo muwezesha kulipwa kiasi hicho anachodai huku akimtaka mganga mfawidhi kuharakisha uhakiki wa nyaraka izo ili aweze kupatiwa haki yake anayostahili ambapo amesisitiza kuwa “Malipo ya Serikali hayawezi kufanyika bila kuwa na nyaraka stahiki, hivyo nyaraka zote zinzotakiwa ziwepo”
Aidha RC Chalamila amemchangia Bi Martha pesa tasilimu milioni 2 za kwake binafsi ili akaongeze mtaji katika biashara zake anazozifanya kwa kuwa ameonyesha kuwa mwanamke mtafutaji licha ya kuwa mjane.
Vilevile RC Chalamila ametoa rai kwa wananchi hasa wale wanaofanya kazi na taasisi mbalimbali za Serikali kuhakikisha wanakuwa na nyaraka stahiki ili kuepuka kuchelewesha malipo yao.
Naye Bi Martha amekiri katika mkataba wake kuna vitu haviko sawa na ameridhika kwa ushauri aliopatiwa na Mkuu wa Mkoa pia amemshukuru kwa kumpatia shilingi milioni 2 kama mtaji wa biashara anayoifanya.
Kwa upande wa Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Amana Dkt Bryson Kiwelu amemshukukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwa karibu na Hospitali hiyo hali inayochangia kwa kiasi kikubwa utoaji wa huduma bora kwa jamii na amemuakikishia kutekeleza maagizo yake kwa wakati.
11 months ago | [YT] | 0
View 0 replies
OTV MEDIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan afuturisha Watoto Yatima na Watoto wenye mahitaji Maalum, Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 3 Machi, 2025.
11 months ago | [YT] | 1
View 0 replies
OTV MEDIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanza kwa mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake Tanzania (Female Future Program) pamoja na Mahafali ya Wahitimu wa Awamu ya 10 ya Mafunzo hayo katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 21 Februari, 2025.
11 months ago | [YT] | 0
View 0 replies
OTV MEDIA
https://youtu.be/L6qMOnthrtw?feature=...
11 months ago | [YT] | 0
View 0 replies
OTV MEDIA
Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Tume ya Rais ya Kutathmini kuhusu masuala ya mgogoro wa ardhi ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na Tume ya Rais ya Kutathmini zoezi la uhamaji wa hiari wa wakazi wa eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 20 Februari, 2025.
11 months ago | [YT] | 0
View 0 replies
OTV MEDIA
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga, leo Februari 18, 2025 amezindua mafunzo ya usimamizi wa vyama vya ushirika kwa maafisa ushirika Kanda ya Kaskazini yatakayo dumu kwa siku 11 ambapo kwa mkoa wa Manyara yatafanyika kwa siku 6 yakihusisha Mikoa ya Manyara, Singida, Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Dodoma.
Mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo maafisa ushirika, uwekezaji na matumizi mifumo ya kisasa (TEHAMA), kuimarisha Maendeleo ya Benki ya ushirika, Uadilifu, Maadili na utunzaji wa Siri pamoja na mambo mengine.
Akizungunza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo RC Sendiga, amewapongeza tume ya maendeleo ya ushirika kwa kuandaa mafunzo hayo kwani yatasaidia kuwajengea uwezo, uadilifu na kufanya kazi kwa kujiamini kwa maafisa ushirika hawo.
Aidha, RC Sendiga, ameiagiza tume ya maendeleo ya ushirika kutatua migogoro iliyopo ndani ya vyama vya ushirika kwani inachelewesha maendeleo na kudumaza vyama vya ushirika.
11 months ago | [YT] | 0
View 0 replies
Load more